Dkt. Chamriho : Mafundi Sanifu wana mchango mkubwa katika ujenzi wa viwanda

0
167

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dkt. Leonard Chamriho amesema fani ya ufundi sanifu ina mchango mkubwa katika ujenzi wa Tanzania ya viwanda.

Akifungua kongamano la siku moja la mafundi sanifu mkoani Dar es Salaam, Dkt. Chamriho amesema, sera ya viwanda inahitaji mchango wa mafundi sanifu katika ujenzi wa viwanda na uendeshaji wa mitambo.

Dkt. Chamriho amesema, uwiano baina ya mafundi sanifu na Wahandisi sio mzuri, na hivyo kuelezea mikakati iliyowekwa na Serikali katika kuongeza idadi ya mafundi wa kada hiyo.

Aidha amewataka mafundi sanifu kutumia weledi katika utendaji wao wa kazi, ili kutimiza azma ya Serikali ya ujenzi wa viwanda.

Awali Mwenyekiti wa bodi ya Usajili wa Wahandisi Nchini (ERB) Profesa Ninatubu Lema alisema kuna upungufu wa mafundi sanifu hapa nchini kutokana na vyuo vingi kujikita katika utoaji elimu ya juu ya fani ya uhandisi pekee.