Kahawa ya Tanzania yazidi kupeta duniani

0
320

Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoshiriki kwenye hafla ya kuonja kahawa inayozalishwa katika nchi mbalimbali za Afrika, hafla iliyofanyika katika jiji la Changsha jimbo la Hunan nchini China.

Mbali na Tanzania, nchi nyingine zilizoshiriki ni Kenya, Uganda, Rwanda na Ethiopia ambapo wageni mbalimbali walipata fursa ya kuonja aina tofauti za kahawa zinazozalishwa katika nchi hizo.

Wakati wa hafla hiyo, Afisa Ubalozi wa Tanzania nchini China, Lusekelo Gwasa alitoa maelezo kuhusu aina mbalimbali za kahawa zinazozalishwa hapa nchini.

Hafla hiyo ya kuonja kahawa inayozalishwa katika nchi za Afrika, kwa upande wa Tanzania inatarajiwa kuongeza fursa ya upatikanaji wa soko la kahawa inayozalishwa nchini, katika soko la China.