Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Profesa Mayunga Nkunya amefariki dunia hii leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili mkoani Dar es salaam.
Taarifa ya kifo cha Profesa Nkunya imetangazwa na Katibu Mtendaji wa TCU Profesa Charles Kihampa.
Profesa Kihampa amesema TCU itaendelea kukumbuka mchango wa Profesa Nkunya uliowezesha kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Tume hiyo.