Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kujitathmini kama anaimudu nafasi hiyo, kutokana na kushindwa kukamilisha utengenezaji wa vitambulisho kwa wakati.
Waziri Simbachawene ambaye yuko kwenye ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Iringa ametoa kauli hiyo baada ya Kaimu Afisa wa NIDA wa mkoa huo Jane Shayo kueleza kuwa, hadi sasa ni asilimia 33 tu ya watu laki nne waliosajiliwa ndio wamepata vitambulisho vya Taifa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita mkoani humo.