Barnaba kufunga ndoa hivi karibuni

0
191

Msanii wa Bongo Fleva Barnabas Elias (Barnaba Classic), amesema anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni. Barnaba amezungumza hayo kupitia kipindi cha Jaramba Serebuka cha TBC1 wakati akijibu swali aliloulizwa sababu za kufanya video ya Cheketua kuwa na mazingira ya kuoa.

“Kwanza mashabiki zangu waelewe kuwa nitaoa hivi karibuni, kwa hiyo nilichokiimba kwenye wimbo wa cheketua kitatokea kwa uhalisia hivi karibuni”, amesema Barnaba.

Barnaba ni miongoni mwa wasanii watakotumbuiza kwenye hafla ya utoaji tuzo kwa wanafunzi wa vyuo vya uandishi wa habari iliyoandaliwa na TBC FM zitakazofanyika tarehe 23 Julai 2021.