Watu binafsi wahamasishwa kununua hisa

0
183

Mrajisi Mkuu wa vyama vya ushirika nchini, Dkt. Benson Ndiege amevitaka vyama vya ushirika nchini, pamoja na watu binafsi kununua hisa ili kuimarisha benki hiyo kuelekea benki ya kitaifa.

Dkt.Ndiege ameyasema hayo mjini Moshi wakati akifungua Mkutano wa 24 wa Benki ya Ushirika mkoani Kilimanjaro, ambao umewakutanisha wanahisa wa benki hiyo kujadili mafanikio na changamoto za benki.

Dkt. Ndiege amesema hatua hiyo itasaidia kuongeza mtaji na kupanua wigo wa umiliki kwa wanachama.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja Mkuu wa kampuni tanzu ya CRDB, Wilson Mnzava, amesema wameanzisha bima ya afya ya kila mwanaushirika ili kuhakikisha wanapata huduma za afya katika hospitali zote nchini.

Tayari Benki ya Ushirika imepata faida ya shilingi Milioni 35, katika robo ya pili ya Machi 2021 ikiwa ni ongezeko la asilimia 52 ikilinganishwa na milioni 23 ya robo ya kwanza.

Sauda Shimbo, Moshi.