Makamu wa Rais hausiki na akaunti hii

0
223

Ofisi ya Makamu wa Rais imesema Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango hausika na ukurasa uliopo kwenye mtandao wa Twitter unaosomeka kwa jina la Dr Philipo Mpango.

Imesema Dkt. Mpango hausiki na ukurasa huo na mambo yote yaliyoandikwa ni ya uzushi.

Katika ukurasa huo umeandikwa ujumbe unaosema ‘Malalamiko yamekuwa mengi kuhusu TOZO mpya LAKINI maendeleo yasiyoumiza. Poleni Watanzania wote na huu ndio muda wa kuanza kuzoea kulipa Kodi kwa ajili ya uchumi wa kweli’.