Waziri Biteko aiweka STAMIGOLD kwenye mizani

0
351

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameuagiza uongozi na wafanyakazi wote wa mgodi wa STAMIGOLD, kujitafakari kama utendaji wao una manufaa kwa Taifa.

Amesema hayo Biharamulo mkoani Kagera katika ziara aliyoifanya ya kutembelea mgodi wa STAMIGOLD ambayo ni Kampuni tanzu ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).

“Mungu amewapa bahati ya kuwa kwenye mgodi huu nawasihi uleeni mgodi huu. Mkiulea na nyinyi utawalea. Shirika hili likifa wengi mtapoteza ajira na kukosa mishahara” ameeleza Biteko akionesha kuchukizwa sana na vitendo vya utoroshaji madini ya dhahabu vinavyofanywa na baadhi ya watumishi wasiowaaminifu.

Aidha, amemuagiza mwenyekiti wa bodi ya STAMICO kuhakikisha anachukua hatua za kiutumishi dhidi yao na wale waliopo mahakamani hatua za ndani zifuatwe za kazi ili wawajibishwe.