Balozi Sefue : Hayati Mkapa aliichukia rushwa

0
158

Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Balozi Ombeni Sefue amemuelezea aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu wa Tanzania Hayati Mzee Benjamin Mkapa kuwa alikuwa kiongozi aliyeichukia rushwa kwa vitendo alipokuwa madarakani.

Akisoma maelezo kuhusu Hayati Mzee Mkapa katika Kongamano la Kumbukizi ya mwaka mmoja tangu kifo cha kiongozi huyo, Balozi Sefue amesema Hayati Mzee Mkapa kamwe hakupenda rushwa katika kipindi chote cha miaka kumi cha uongozi wake.

Amesema Hayati Mzee Mkapa aliunda Tume ya Warioba ambayo iliangalia mwenendo wa rushwa nchini, na kuchukua hatua mbalimbali za kukabiliana na vitendo vya rushwa.

Balozi Sefue amesema sera ya Hayati Mkapa ya uwazi na ukweli ilisaidia kuonesha namna alivyoichukia rushwa na kuipinga kwa vitendo, ambapo pia alianzisha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini.