Tanzania na Morocco kushirikiana katika sekta mbalimbali

0
201

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye anaendelea na ziara yake nchini Morocco, kwa nyakati tofauti amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika wa nchi hiyo Nasser Bourita, pamoja na Waziri Mkuu Saad Dine El Otmani.
 
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika jijini Rabat, Viongozi hao wamezungumzia namna ya kuimarisha ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili uliodumu kwa muda mrefu.
 
Waziri Mkuu Majaliwa amesisitiza umuhimu wa Tanzania na Morocco kuendelea kushirikiana katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na Elimu, Kilimo, Utalii, Nishati na Uvuvi.
 
Katika ziara yake nchini Morocco, Waziri Mkuu Majaliwa ameongoza na Viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda, Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Zanzibar – Leila Muhamed Mussa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk.