Ulega ataka kumalizika kwa migogoro

0
288

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega ameusisitiza uongozi wa Mkoa wa Pwani kutumia mkakati wa uvunaji wa mifugo kama mkakati wa kumaliza migogoro ya wafugaji na wakulima pamoja na kuondokana na tatizo la uhaba wa malighafi katika viwanda vya kuchakata nyama mkoani humo.

Naibu Waziri Ulega amesema hayo alipokutana na uongozi wa mkoa huo ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge, wakati akitoa taarifa ya ziara yake ya kikazi ya siku mbili Mkoani Pwani na kufafanua kuwa ni vyema Mkoa ukafanya tathmini ya kina kwa kuunda kamati maalum ili kutafuta suluhu ya migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akiwa katika Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) iliyopo Wilaya ya Kibaha, Mkoani Pwani ameagiza uongozi wa Taasisi hiyo kuhakikisha chanjo zinazozalishwa na taasisi hiyo zinawafikia wafugaji waliopo vijijini badala ya kuanza kufikiria kusambaza chanjo hizo nje ya nchi.

Ulega amesema kuna mifugo mingi kama kuku, ng’ombe na mbuzi wanaokufa kwa kuwa wafugaji hawajui kama kuna chanjo zinazozalishwa hapa nchini ingawa kuna maeneo mengine chanjo hizo hazijafika kabisa.

Ulega ametembelea pia kiwanda cha kuzalisha chanjo za mifugo cha HESTER kilichopo Wilayani Kibaha na kujionea namna kiwanda hicho kinavyozalisha chanjo ambazo zitakuwa zikiuzwa ndani na nje ya nchi