Sanga aendelea na ziara kijiji kwa kijiji

0
120

Mbunge wa jimbo la Makete mkoani Njombe, Festo Sanga ameendelea na ziara ya kijiji kwa kijiji katika jimbo lake, lengo likiwa ni kusikiliza kero za Wananchi.

Akiwa katika kijiji cha Usagatikwa kata ya Tandala, Sanga amekutana na changamoto ya barabara kujengwa chini ya kiwango, na kutaka barabara hiyo kutopokelewa hadi hapo Mkandarasi atakapoweke kifusi sahihi, makaravati na mifereji ya maji.

Sanga pia amechangia mifuko mia moja ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa zahanati.