Biashara zaruhusiwa soko dogo Kariakoo

0
121

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla ameruhusu kuanza kwa shughuli za biashara kwenye soko dogo la Kariakoo, kutokana na eneo hilo kutoathiriwa na moto.
 
Makalla amesema hayo alipotembelea soko hilo, ambapo pia ametaka Wafanyabiashara wote wanaoendesha biashara zao kwenye eneo la hifadhi ya barabara ya kuingia sokoni hapo kuondoka ili barabara ibaki wazi.
 
Ameshauri kwa wakati huu ambao hali ya usalama katika soko kubwa haijakaa sawa, Wafanyabiashara wachukuwe mali zao na kuhamia soko la Kisutu na Machinga Complex hadi hapo marekebisho yatakapofanyika.
 
Kuhusu soko la Shimoni ambalo inaelezwa halijaathiriwa kwa kiasi kikubwa na moto, Makalla amesema kutokana na mfumo wa umeme kuharibika katika soko hilo , ni vema ufanyike utaratibu ili Wafanyabiashara wakachukue bidhaa zao na kuhamia soko la Machinga Complex na Kisutu.