Uchafuzi chanzo cha maji wamkera Waziri

0
128

Waziri wa Maji Jumaa Aweso amemuagiza mkuu wa wilaya ya Lushoto mkoani Tanga Kalist Lazaro kukutana na Watendaji wa wizara ya Madini, ili kutatua changamoto ya uchafuzi wa mazingira katika chanzo cha maji cha Kindoi kilichopo wilayani Lushoto mkoani Tanga.

Waziri Aweso ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake katika chanzo hicho cha maji, kwa lengo la kukagua uchafuzi mazingira ambao umekuwa ukiendelea katika eneo hilo.

Chanzo hicho cha maji cha
Kindoi ambacho kinatiririsha maji yake na kuwafikia pia Wakazi wa Korogwe, kinadaiwa kuchafuliwa na wachimbaji wadogo wa madini ambao wamekuwa wakiendesha shughuli zao katika eneo hilo wakiwa na leseni inayotambuliwa na Serikali.

Kwa mujibu wa wizara ya Maji, mpaka sasa Wakazi wa wilaya ya Lushoto wanapata maji safi na salama kwa asilimia sitini.