STAMICO yajivunia kiwanda cha kusafisha dhahabu cha Mwanza

0
138

Shirika la Taifa la Madini (STAMICO) limesema kiwanda cha kusafisha dhahabu cha Mwanza Precious Metal Refinery kitasaidia kuongeza thamani ya madini ya dhahabu yanayozalishwa hapa nchini na kumkomboa mchimbaji mdogo wa madini hayo.

Akizungumza na TBC jijini Dar es salaam, Meneja Masoko na Uhusiano wa STAMICO Geofrey Meena amesema, kiwanda hicho kitawasaidia wachimbaji wadogo wa dhahabu kupata soko la kuuzia madini yao na pia kuyaongezea thamani.

Meena ameongeza kuwa, kiwanda hicho kilichozinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kitasaidia ukuaji wa sekta ya madini hasa dhahabu, kwani kwa sasa kitasafisha dhahabu yote hapahapa nchini na kuongeza ajira kwa Watanzania.

Kuzinduliwa kwa kiwanda hicho cha kusafisha dhahahu cha Mwanza Precious Metal Refinery
kumekuwa mkombozi kwa wachimbaji wa madini hapa nchini, ambapo kwa sasa dhahabu yote inayozalishwa itaongezewa thamani nchini kabla ya kuuzwa nje.