Simba SC imetwaa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2020/21 kwa mara ya nne mfululizo.
Simba imekuwa bingwa baada ya kufikisha alama 79 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote, huku bado ikiwa na michezo miwili kibindoni.
Wekundu wa msimbazi wametwaa ubingwa;
🏆 2017-18
🏆 2018-19
🏆 2019-20
🏆 2020-21
Mbali na ubingwa, Nahodha wa Simba, John Bocco ndiye anaongoza kwa ufungaji magoli akiwa na magoli 15 hadi sasa akifuatiwa Prince Dube wa Azam FC mwenye magoli 14.
Mwamba wa Lusaka, Clatous Chama yeye anaongoza kwa usaidizi wa magoli (assists), ambapo ametoa usaidizi kwenye magoli 15.
Je! Simba itaweza kufanya kama ilivyofanya mwaka 1976 hadi 1980 kwa kutwaa ubingwa wa ligi mara tano mfululizo? Msimu wa 2021/22 utatoa majibu.
