Muhubiri Amritzer amwaga sifa kwa Rais Samia Suluhu Hassan

0
209

Muhubiri wa Kimataifa wa huduma ya SOS Adventures kutoka nchini Sweden, Johannes Amritzer amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuijenga nchi katika msingi wa umoja na mshikamano uliohasisiwa na watangulizi wake.

Akizungumza na Waandishi wa habari mkoani Kigoma, mhubiri huyo ambaye anatarajia kufanya tamasha kubwa la maombi kuanzia kesho mkoani humo amesema kuwa, Tanzania imeendelea kuwa nchi ya mfano kwa kudumisha amani, umoja na mshikamano miongoni mwa Wananchi wake pasipokujali madhehebu yao ya dini.

Aidha Amritzer ameipongeza Serikali kwa kuendelea kudhibiti vitendo viovu ikiwemo rushwa na matumizi mabaya ya madaraka, huku akisisitiza kuwa Mungu anapendezwa na Viongozi wanaosimamia matendo mema yenye kuleta maendeleo kwa Wananchi.

Mhubiri huyo kutoka nchini Sweden atakuwa mkoani Kigoma kwa muda wa siku tano kwenye tamasha la maombi linalotarajia kuanza kesho katika viwanja vya community Centre vilivyopo katika Manispaa ya Kigoma – Ujiji.