Chakula chenye sumu chadaiwa kuua watoto

0
164

Watoto wawili, wakazi wa kata ya Ikobe wilayani Mbogwe mkoani Geita wamefaiki dunia
baada ya kula chakula kinachosadikiwa kuwa na sumu.

Watoto wengine 15 wamelazwa katika kituo cha afya cha Iboya baada ya kula chakula hicho.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Geita – Henry Mwaibambe amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Amesema watoto hao walikula chakula kilichoandaliwa siku ya harusi iliyofanyika katika kata hiyo ya Ikobe.

Kwa mujibu wa Kamanda Mwaibabe, uchunguzi zaidi kuhusu tukio hilo unaendelea.