Zuma apinga adhabu mahakama

0
156

Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amesema kuwa alichokuwa akikipinga katika utawala wa ubaguzi wa rangi (apartheid) ndicho kilichotendekea kwake alipohukumiwa kwenda jela miezi 15.

Zuma ameeleza kushangazwa na kupewa adhabu hiyo pasipo kuendeshwa kwa kesi na kudai kuwa mahakama inatumiwa na wapinzani wake wa kisiasa kujipatia umaarufu.

Kiongozi huyo kutoa ANC alikuwa amepewa hadi Julai 4 mwaka huu awe amejisalimisha mwenyewe tayari kutumikia adhabu hiyo baada ya kukutwa na hatia ya kudharau amri ya mahakama.

Hata hivyo jana alisema hatotii amri hiyo ya kujisalimisha, kauli iliyokuja baada ya Mahakama ya Katiba kukubali kusikiliza rufaa yake inayotaka kutenguliwa kwa hukumu hiyo.

Mamia ya wafuasi wake wamepiga kambi katika nyumba yake kwa kile walichoeleza kuwa ni kumlinda asikamatwe, mkusanyiko ambao ni kinyume na kanuni za kupambana na ugonjwa wa #COVID19 nchini humo.

Zuma alipewa adhabu hiyo kwa kushindwa kuitikia wito wa mahakama wa kufika mahakamani kujibu kesi ya rushwa.