Serikali kuwasaidia wawekezaji wa viwanda

0
351

Waziri wa Viwanda na Biashara, Profesa Kitila Mkumbo amesema atakaa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Selemani Jafo ili kwa pamoja watatue changamoto za viwanda vinavyozalisha bidhaa kwa kutumia mabaki ya madini ya shaba.

Waziri Mkumbo ametoa ahadi hiyo mara baada ya kutembelea kiwanda cha OK Plastic kinachozalisha bidhaa kwa kutumia mabaki ya shaba mkoani Dar es Salaam.

Akiwa kiwandani hapo Prof. Mkumbo amejionea namna nyaya na bidhaa nyingine zinavyozalishwa kwa ubora wa hali ya juu na ametoa rai kwa Watanzania kuendelea kutumia bidhaa mbalimbali zinazozalishwa hapa nchini kwani zimekuwa na ubora wa kimataifa

Waziri Mkumbo amefanya ziara hiyo kwa lengo la kujionea uzalishaji katika viwanda vya hapa nchini na kusikiliza changamoto.