Mwili wa aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale utaagwa leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam ambapo watumishi wa TANROADS, Wizara ya Ujenzi na wananchi kwa ujumla watatoa heshima zao za mwisho.
Baada ya shughuli hiyo mwili huo utapelekwa Kimara Temboni nyumbani kwa Mfugale.
Baada ya misa takatifu siku ya Jumamosi Julai 3, 2021 mwili wa Mfugale utasafirishwa kwenda Ifunda mkoani Iringa ambapo unatarajiwa kuwasili Julai 4 na maziko yatafanyika Julai 5, 2021 nyumbani kwake Ifunda.
Mfugale alifariki dunia Jumanne Juni 29, 2021 saa 5 asubuhi katika hospitali ya Benjamin Mkapa.