Rais apokea taarifa ya maandalizi ya sensa 2022

0
311

Rais Samia Suluhu Hassan amepokea taarifa ya maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika mwezi Agosti, 2022 kutoka kwa Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa.

Dkt. Chuwa amesema Sensa ya mwaka 2022 itatumia teknolojia ya kisasa ya Kidijitali chini ya mfumo ulipo wa Serikali katika ngazi zote za Utawala kwa pande zote za Muungano.

Aidha, amesema Sensa ya majaribio itafanyika mwezi Agosti mwaka huu (2021) katika mikoa saba kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar.