Basi laacha njia na kugonga nyumba

0
149

Basi la abiria, mali ya kampuni ya Ulama lenye namba za usajili T330 DGB lililokuwa likisafiri kutoka Mwanza kuelekea mkoani Arusha, limeacha njia na kugonga nyumba ya Regina Masanja iliyokuwa jirani na barabara katika eneo la Mkolani mkoani Mwanza.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza, Ramadhani Ng’anzi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kuwa, wakati ajali hiyo inatokea basi hilo lilikiwa na zaidi ya abiria hamsini.

Amesema katika ajali hiyo watu 12 wamejeruhiwa, na kwamba uchunguzi wa awali umebaini  kuwa ajali hiyo imesababishwa na hitilafu kwenye mfumo wa kuongozea basii hilo.

Kamanda Ng’anzi amesema majeruhi wote wanaendelea na matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa Mwanza, Sekou – Toure pamoja na hospitali ya wilaya nyamagana.