Ethiopia kusimamisha mapigano Tigray

0
168

Serikali ya Ethiopia imetangaza kusimamisha mapigano dhidi ya wapiganaji wa jimbo la Tigray, hatua ambayo imepokewa kwa shangwe na wapiganaji nchini humo.

Jeshi la Ethiopia lilivamia Jimbo la Tigray kwa madai ya kuzima uasi wa wapiganaji wa jimbo hilo ambalo linadai haki zaidi katika uwakilishi wa serikali kuu ya Shirikisho la Ethiopia.

Katika mapigano kati ya pande hizo mbili maelfu ya wananchi wa jimbo la Tigray wameyakimbia makazi yao huku wengine wakiuawa na mali kadhaa ikiwemo mashamba na majengo zikiharibiwa.