PAC yapongeza uchambuzi wa ripoti ya CAG

0
170

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imepongeza uchambuzi wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa kuandikwa kwa lugha rahisi, iliyofanywa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Wajibu ­- Institute of Public Accountability, hatua itakayorahisisha wananchi kuielewa ripoti husika.

Hayo yamesemwa jijini Dodoma katika hafla ya uzinduzi wa ripoti za uwajibikaji mwaka 2019/2020.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Naghenjwa Kaboyoka amesema taasisi ya Wajibu imekuwa msaada kwa wananchi kwakuwa uchambuzi wa ripoti ya CAG unafanywa kwa kina zaidi hata yale ambayo wabunge hawapati nafasi ya kuyaongea bungeni wananchi wanayapata kupitia ripoti za Wajibika.

Mkurugenzi wa Wajibika, Ludovick Uttoh, CAG Mstaafu, ameiomba serikali kuendelea kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato ili wananchi waweze kunufaika na rasilimali za taifa lao.

’’Ninaiomba wasilegeze, waendelee kusimamia mapato yanayopatikana kutoka vyanzo mbalimbali ili vitumike kwa manufaa ya kuwaletea maendeleo Watanzania,” amesisitiza Uttoh.

Edigar Nkilabo – Dodoma