waokoaji wanaendelea na juhudi za kuwatafuta watu walionaswa katika vifusi baada ya jengo moja na ghorofa kuporomoka huko Miami katika Jimbo la Frolida
Watu tisa wamekufa huku wengine wakijeruhiwa ambapo baadhi yao wanasadikiwa kuwa wamenasa katika vifusi vya jengo hilo.
Meya wa Miami Daniella Cava amesema idadi ya watu waliokufa huenda ikaongezeka kwani zaidi ya watu 150 hawajulikani walipo kufuatia kuanguka kwa jengo hilo lenye ghorofa Kumi na Mbili Alhamisi iliyopita.
Jana Jumapili waumini wa dini ya Kikristo wameshiriki ibada makanisani kuwaombea wahanga wa tukio hilo.