Vyombo vya habari vyatakiwa kuendelea kupaza sauti juu ya madhara ya dawa za kulevya

0
180

Vyombo vya habari nchini vimetakiwa kuendelea kupaza sauti juu ya matumizi ya dawa za kulevya nchini na kutoa taarifa muhimu za kuelimisha umma kuhusu madhara ya matumizi ya dawa hizo

Akitoa maagizo hayo Waziri wa mambo ya ndani ya nchi George Simbachawene amewataka wananchi kutoa taarifa kwa vyombo husika kuhusu wafanyabiashara wa dawa za kulevya nchini

Katika hotuba ya mgeni rasmi Waziri Simbachawene amesisitiza na kutoa rai kwa wadau kuwasaidia vijana walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya ikienda sambamba na kuwaimarisha kiuchumi ili wasirudi tena kutumia dawa hizo.

Maadhimisho hayo ya siku ya kupambana na dawa za kulevya duniani yaliyofanyika katika uwanja wa Nyerere Square Jijini Dodoma yamefikia kilele hii leo na kufungwa rasmi na Waziri wa mambo ya ndani ya nchi George Simbachawene akimuwakilisha mgeni rasmi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa