Mkinga aagwa Dar, kuzikwa Chato

0
141

Mwili wa Mwandishi wa Habari Mkinga Mkinga aliyefariki dunia mkoani Dar es salaam, umeagwa hii leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja mkoani Dar es salaam.

Mwili wa Mkinga ambaye alikuwa ni mmoja wa Wahariri wa gazeti la Jamhuri umeagwa na ndugu, jamaa na marafiki wakiongozwa na wanataaluma wa Habari.

Baada ya kuagwa Dar es salaam, mwili wa Mkinga utasafirishwa kesho Jumamosi kwa ndege kwenda wilayani Chato mkoani Geita, kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu.

Mkinga alifariki dunia usiku wa kuamkia tarehe 24 mwezi huu katika hospitali ya Taifa Muhimbili mkoani Dar es salaam, alikokuwa akipatiwa matibabu.