Mtanzania atunukiwa nishani na Rais wa Ufaransa

0
178

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amemtunukia Balozi Mstaafu Radhia Msuya wa Tanzania, nishani ya “National Order of Merit”.

Balozi Msuya
amevikwa nishani hiyo jijini Dar ss Salaam na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederick Clavier kwa niaba ya Rais Macron.

Balozi Msuya ametunukiwa nishani hiyo kutokana na mchango wake katika kuimarisha uhusiano wa Tanzania na Ufaransa wakati akiwa Mkurugenzi wa Ulaya na Amerika katika wizara ya Mambo ya Nje (2006-2010).

Ametambuliwa kwa mchango mahsusi alioutoa wakati Ufaransa ilipokuwa Rais wa Umoja wa Ulaya.

Nishani hiyo ilianzishwa mwaka 1963 kwa nia ya kutambua mchango wa watunukiwa wake katika kuendeleza ushirikiano na Ufaransa hasa katika ustawi wa dunia. …