Serengeti Boys bingwa Ukanda wa Tano Afrika

0
1227

Timu ya Taifa ya soka ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 (Serengeti boys) imetwaa ubingwa wa soka kwa ukanda wa Tano wa Afrika baada ya kuilaza Angola kwenye mchezo wa fainali kwa penati sita kwa tano.
Mchezo huo wa fainali umefanyika katika mji wa Gabarone nchini Bostwana.
Awali Serengeti Boys na timu hiyo ya Angola zilimaliza mchezo huo kwa sare ya bao moja kwa moja ndani ya kipindi cha dakika Tisini na hivyo kuamuliwa kupigwa kwa mikwaju ya penati.
Kocha wa Serengeti Boys, -Oscar Mirambo amesema kuwa ubingwa huo umeongeza chachu kwenye timu yake katika kujiandaa na michuano ya Afrika itakayofanyika nchini mwaka 2019.
Kwa upande wake nahodha wa Serengeti Boys, – Moris Abraham amesema kuwa walijiandaa vema ndio maana wameweza kuibuka washindi kwenye fainali hiyo.
Serengeti Boys na timu hiyo ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ya Angola zilikuwa kwenye kundi moja, ambapo katika mchezo wa hatua ya makundi Angola iliifunga Serengeti Boys na kwenye mchezo wa fainali Serengeti Boys imelipa kisasi na kutwaa ubingwa.