Kardinali Pengo apongezwa kwa utumishi kwa kanisa

0
233

Askofu wa Jimbo Katoliki la Mpanda, Mhashamu Eusebius Nzigirwa amesema ubunifu wa Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo umelifanya jimbo hilo kujikusanyia zaidi shilingi bilioni 3 kwa ajili ya tegemeza Jimbo na kuondokana na utegemezi katika kuwahudumia mapadre na waumini wake.

Askofu Nzigirwa ametoa kauli hiyo wakati wa ibada ya Misa Takatifu ya Jubilei ya Miaka 50 ya Upadre ya Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Pengo iliyofanyika katika viwanja vya Msimbazi jijini Dar es Salaam.

Katika mahubiri yake Nzigirwa amebainisha kuwa awali utaratibu wa tegemeza Jimbo ulioanzishwa na Kardinali Pengo Jimbo hilo lilijikusanyia shilingi milioni 17 tuu kwa mwaka kiasi ambacho hakikutosha kuratibu shughuli mbalimbali za kanisa ikiwemo mahitaji ya mapadre na waseminari wadogo.

“Kardinali Pengo mi zaiwadi ambayo Mungu ameitoa kwa makusudi yake kwa ajili ya waumini wa Jimbo Kuu la Dar es Saalam, hivyo anapoazimisha miaka 50 ya upadre tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa ajili yake maisha yake,” amesema Askofu Nzigirwa

Pia amebainisha kuwa miongoni mwa mafanikio mengine yaliyofanikishwa na Mwadhama Polycarp Pengo ni pamoja na kuwaunganisha mapadre wa Jimbo hilo na mashirika kuwa kitu kimoja.

Kwa Upande wake Balozi wa Baba Mtakatifu nchini Tanzania, Merek Solczynski amempongeza Kardinali Pengo kwa juhudi zake nyingi katika utumishi wake wa kulihudumia kanisa na jamii kwa ujumla.