Serikali yaiimarisha Hospitali ya Bugando

0
205

Ikiwa leo ni Siku ya Seli Mundu (Sickle Cell) Duniani, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi amezindua mashine kubwa yakupima magonjwa yote mwilini ya MRI katika Hospitali ya Kanda, Bugando mkoani Mwanza.

Akikabadhi mashine hiyo Prof. Makubi amesema kipaumbele ni wananchi kupewa elimu kuhusiana na ugonjwa huo.

Amesema kuwa Tanzania ni nchi ya nne kwa kuwa na watu wengi wenye ugonjwa wa seli mundu ikiwa na wagonjwa 2,000, ambapo Kanda ya Ziwa inaongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Bugando, Fabian Masaga amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wakupeleka mashine hiyo hospitalini hapo.

Mashine hiyo ina uwezo wa kupima magonjwa katika nyanja mbalimbali ikiwemo magonjwa ya ubongo na tezi dume.

Maadhimisho ya Siku ya Seli Mundu kitaifa yamefanyika mkoani Mwanza.