Mgumba awaonya wala fedha

0
209

Mkuu wa mkoa wa Songwe Omary, Mgumba amewaonya Watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Momba wenye tabia ya kutumia vibaya fedha za makusanyo ya ndani kuacha mara moja.

Mgumba ametoa onyo hilo wakati akizungumza na Viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Momba, katika Baraza maalum la Madiwani la wilaya hiyo linalokutana kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Kwa miaka mitatu mfululizo, halmashauri ya wilaya ya Momba imekuwa ikipata hati chafu, hivyo Mgumba amewaagiza maafisa tarafa kukusanya taarifa za mapato katika kila kata kila siku, lengo likiwa ni kudhibiti mianya ya ulaji wa fedha hizo.

Amesema taarifa hizo zitasaidia kupunguza matumizi mabaya ya fedha za Serikali.

Mgumba pia amemuagiza Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Momba, Adrian Jungu kutoa taarifa za watumishi ambao wamekua sababu ya halmashauri hiyo kupata hati hizo chafu mfululizo.