Hatima ya Sethi kujulikana leo

0
278

Mshtakiwa namba mbili katika kesi ya uhujumu uchumi ya mwaka 2017 anayedaiwa kuisababishia Serikali hasara ya mabilioni ya fedha Habinder Sethi imeanza kunguruma katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mkoani Dar es Salaam mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo Huruma Shaidi.

Hukumu ya kesi hiyo inatarajiwa kutolewa hii leo baada ya mshitakiwa huyo siku za hivi karibuni kuandika barua kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ili kufanya makubaliano ya kukiri mashtaka yanayomkabili.

Usikilizwaji wa kesi hiyo unaongozwa na jopo la mawakili wa Serikali Martenus Marando, Wakili Mkuu wa Serikali Renatus Mkude wakisaidiwa na Wankyo Simon ambaye ni Wakili Mwandamizi wa Serikali.