Rais Edgar Lungu wa Zambia amewahakikishia Wananchi wa nchi hiyo kuwa hali yake ya kiafya inaendelea vizuri baada ya kujisikia kizunguzungu na kuanguka hadharani hapo jana, alipokuwa akihudhuria siku ya Majeshi ya Taifa hilo.
Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Zambia imeeleza kuwa, Rais Lungu anaendelea na utekelezaji wa majukumu yake kama kawaida.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais Lungu alirejea katika hali yake ya kawaida mara baada ya tukio hilo la kuanguka katika mji mkuu wa Zambia, Lusaka.
Hii ni mara ya pili kwa Rais Lungu kupata tatizo hilo hadharani, ambapo kwa mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2015.
Rais Lungu anatarajiwa kuwania kiti cha Urais kwa kipindi kingine, katika uchaguzi utakaofanyika Agosti 12 mwaka huu.