Chongolo: Madiwani kupimwa kwa vikao

0
249

Na Bertha Mwambela, Tanga

Madiwani nchini wametakiwa kuhudhuria vikao vya shina vinavyofanyika kikatiba kila mwezi, ili waweze kufahamu changamoto za Wananchi na kuzitatua.

Kauli hiyo imetolewa mkoani Tanga na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo, wakati alipokua akizungumza na Wananchi na Wanachama wa chama hicho katika kata ya Magila Gereza wilayani Korogwe.

Amesema msingi wa chama upo kwenye mashina, hivyo ni wazi kuwa kila diwani anapaswa kuhudhuria vikao hivyo.

“Naomba niseme wazi kuwa utakapofika wakati wa uchaguzi tutawapima kulingana na utekelezaji wa majukumu kwenye maeneo yenu. Na miongoni mwa majukumu ni kuhudhuria vikao vya shina ili kufahamu changamoto za Wananchi na kuzitatua.”amesema Chongolo

Kikatiba vikao hivyo vya shina hufanyika kwa mwezi mara moja kwa miezi yote 12, na kikao kimoja kati ya hivyo ni maalum kwa ajili ya mkutano mkuu.