Mapigano yasitishwa Hodeida

0
1517

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, – Mike Pompeo amesifu usitishwaji wa mapigano katika mji wa bandari wa Hodeida uliopo nchini Yemen.

Hatua hiyo ya usitishwaji mapigano imefikiwa baada ya kumalizika kwa mazungumzo ya kutafuta amani nchini Yemen yaliyokuwa yakifanyika nchini Sweden katiĀ  ya waasi wa Houthi na wawakilishi wa serikali.

Pompeo amesema kuwa licha ya kuwa bado yanahitajika majadiliano zaidi baina ya pande hizo mbili, lakini masuala yaliyofikiwa hivi karibuni kati ya pande hizo niĀ  muhimu.

Amempongeza mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen, – Martin Griffiths pamoja na mataifa Sweden na Saudi Arabia kwa kuwezesha kufanyika kwa mazungumzo hayo.