Masisi wa Botswana atua nchini

0
196

Rais Mokgweetsi Masisi wa Botwana amewasili nchini hii leo, kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere mkoani Dar es salaam , Dkt. Masisi amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula.

Akiwa hapa nchini pamoja na mambo mengine, Rais Masisi atakutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu jijini Dar es salaam.