New Victoria na New Butiama zazinduliwa

0
142

Rais Samia Suluhu Hassan amezindua Meli ya New Victoria Hapa Kazi Tu na New Butiama Hapa kazi tu, ambazo zitakuwa zikitoa huduma ya usafiri katika eneo la ziwa Victoria.

Rais Samia Suluhu Hassan amezindua meli hizo katika siku ya tatu na ya mwisho ya ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza, ziara iliyokuwa na lengo la kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na Wakazi wa mkoa huo.

Meli hizo mbili zimezinduliwa baada ya kukamilika kwa ukarabati mkubwa ulioanza mwezi machi mwaka 2019, ambapo kazi kubwa zilizofanyika ni pamoja na kuweka mitambo mipya ndani ya meli hizo, kuweka vifaa vipya vya kuendeshea na kuweka vifaa vipya vya usalama.

Tayari meli hizo zimefanya kazi kwa kwa muda wa mwaka mmoja kwa majaribio, na kwa sasa Wakandarasi wanajianda kuzifanyia ukaguzi wa mara ya mwisho ili ziweze kupata cheti cha ubora na kuanza rasmi kutoa huduma za usafiri baada ya ukarabati huo mkubwa.