Miss Rwanda 2016 atua nchini

0
2654

Aliyewahi kuwa Miss Rwanda mwaka 2016 Jolly Mutes amewasili nchini kwa ajili ya kutoa hamasa kwa walimbwende wa kitanzania wanaowania taji la urembo la Afrika Mashariki mwaka huu.

Mlimbwende huyo ambaye kwa sasa ni Makamu wa Rais wa Kampuni inayoandaa shindano la Miss East Afrika amesema fani hiyo ina fursa nyingi za kuitangaza nchi kimataifa lakini pia kusaidia jamii.

Mratibu wa shindano hilo hapa nchini Mariam Ikoa anasema Jolly Mutes atakuwa nchini kwa majuma mawili ili kuhamasisha walimbwende wa Tanzania kushiriki mashindano hayo na kufaidika na fursa zilizopo katika fani hiyo.

Pamoja na mambo mengine Miss Mutes atashuhudia maandalizi ya mashindano ya urembo ya afrika mashariki mwaka 2021 na pia atafanya makongamano kadhaa na walimbwende wa Tanzania.