Rais Samia Suluhu Hassan afanya uteuzi wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu)

0
184

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Jaffar Haniu kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu).

Kabla ya uteuzi alikuwa Mtendaji Mkuu wa vyombo vya habari vya Africa Media Group Limited.

Haniu anachukua nafasi ya Gerson Msigwa ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali.

Uteuzi huo umeanza leo Juni 9, 2021