Siku tatu za ziara ya Rais mkoani Mwanza

0
153

Rais Samia Suluhu Hassan atanatarajiwa kufanya ziara ya siku tatu mkoani Mwanza kuanzia Juni 13 hadi 15 mwaka huu ambapo pamoja na mambo mengine atafungua miradi ya maendeleo.

Akiwa ziarani anatarajiwa kuweka jiwe la msingi katika jengo la Benki Kuu ya Tanzania (BOT) na kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigongo – Busisi (3.2km) ambalo ujenzi wake unagharimu shilingi bilioni 699.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Albert Chalamila amesema Rais Samia Suluhu Hassan pia atazindua miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa maji wilayani Misungwi uliogharimu shilingi bilioni 13.7.

Aidha, Chalamila amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika ziara hiyo ya Rais, ambayo itakuwa ziara yake ya kwanza mkoani humo tangu alipoapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Machi 19, 2021.