Kifuu cha nazi kinaweza kukuletea mapato mazuri kupitia njia mbalimbali za ubunifu kwa kuongezea ubora na thamani.
Ukiachana na faida za mafuta ya nazi ambayo wengi hutumika kama dawa ya magonjwa ya ngozi, upande mwingine kupitia vifuu vya nazi kuna faida kubwa kwa matumizi kama kutengeneza vitu vya sanaa.
Kutengeneza vyombo kama vile bakuli.
Kuna muda sio lazima utumie vyombo vya kawaida, unaweza kuboresha kifuu cha nazi na kukifanya kama bakuli na ukapakulia chakula chako.
Vile vile kifuu cha nazi kinaweza kutengenezwa kuwa vijiko au nyuma
Kupandia maua
Kifuu cha nazi na mwonekano wake mzuri unaweza kutumia kamba kuning’iniza na kutumia kipande maua na kupendezesha nyumba yako.
Kutengeneza pochi
Hakika ni ubunifu wa madoido yake kifuu cha nazi kinaweza kubadilisha mwonekano na kuwa pochi nzuri yenye mpangilio mzuri
Kutengeneza vihifadhio
Kweli kila kitu mipango…!!! Kifuu cha nazi ukisafisha vizuri na kuweka kwa mpangilio mzuri unaweza kukitumia kupangilia na kuhifadhi vitu vyako kama hereni, sabuni, vipodozi, pesa na pini za hijabu.
Kutengeneza mapambo
Kifuu cha nazi kinaweza kutumika kutengeneza mapambo kama hereni, bangili, vifungo na cheni
Kuremba ukuta
Vifuu vya nazi na ugumu wake vikipangiliwa vizuri ukutani ni nakshi ya nyumba.
Je sasa utatupa kifuu cha nazi? Tupe ubunifu wako ambo hatujaweka kwenye horodha yetu.
Picha @Pinterest
https://www.instagram.com/judith.ene.laizer/