Benki ya Dunia yaipa Tanzania trilioni 2

0
295

Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Dunia imetoa mkopo wa masharti nafuu kwa Serikali ya Tanzania jumla ya dola za kimarekani bilioni 1.017 (shilingi trilioni 2.3391) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.

Fedha hizo zitatumika kwenye miradi mbalimbali ikiwemo Roads to Inclusion and Socio -economic Opprtunities (RISE), Higher Education for Economic Transformation Project (HEET), mradi wa Digital Tanzania Project (DTP), na mradi wa Zanzibar Energy Sector Transformation and Access Project.

Dk. Mwigulu ameitaja miradi mingine kuwa ni mradi wa RISE ambao utasaidia kuboresha barabara za vijijini na kutoa fursa za ajira takribani ajira 35,000 kwa wananchi waliopo katika vijiji nufaika pamoja na kujenga uwezo wa usimamizi endelevu wa barbara za vijijini kwa kuhusisha njia shirikishi za jamii.