Majangili tafuteni kazi nyingine

0
174

Bunduki 24, meno ya tembo manne na watuhumiwa 91 wamekamatwa katika operesheni iliyofanywa na Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA) kwa kipinndi cha kuanzia Aprili hadi Juni, 2021 katika mapori ya akiba na hifadhi za jamii mikoa ya Katavi, Kigoma na Tabora.

Kamanda wa Uhifadhi wa Kanda ya Magharibi (inayohusisha mikoa hiyo), Bigilamungu Kagoma amewakata wanaojihusisha na ujangili kutafuta kazi nyingine vinginevyo wataendelea kukumbana na mkono wa vyombo vya ulinzi na usalama.