Rais Samia Suluhu Hassan amesema Balozi na Taasisi za kimataifa zinaruhusiwa kuleta chanjo nchini za ugonjwa wa corona kwa ajili ya kuwachanja raia na watumishi wake, ili kuendana na taratibu za nchi zao na taasisi hizo pamoja na kuondoa kadhia wanazopata katika utendaji wa kazi zao kutokana na kutochanjwa.
Rais Samia Suluhu Hassan ameyasema hayo wakati akipokea mapendekezo ya mpango kazi wa kutafuta rasilimali kwa ajili ya utekelezaji wa mpango mkakati wa Taifa wa kukabiliana na janga la corona na mapendekezo ya mpango kazi wa uratibu na utoaji chanjo ya ugonjwa huo.
Mapendekezo hayo yamewasilishwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu Chamwino mkoani Dodoma na Kamati ya Wataalam aliyoiunda kwa ajili ya kuishauri Serikali juu ya kukabiliana na ugonjwa huo.