TBC yaanza maandalizi ya mechi dhidi Bunge

0
158

Timu ya mpira wa miguu ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) TBC Warriors imepokea seti ya jezi kutoka kampuni ya Sportpesa, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo kati ya timu hiyo na timu ya Bunge.

Akikabidhi jezi hizo katika ofisi za TBC Mikocheni mkoani Dar es salaam, Mkurugenzi wa Utawala na Uendeshaji wa Sportpesa Tarimba Abbas amesema kuwa kampuni hiyo imetoa jezi hizo ili kuendelea kudumisha uhusiano kati ya tasisi hizo mbili.

Kwa upande wake Mratibu wa miradi wa TBC Gabriel Nderumaki amesema kuwa vifaa vilivyotolewa na Sportpesa kwa TBC vitaleta chachu ya ushindi wakati wa mechi dhidi ya TBC Warriors na Bunge SC.

Mechi kati ya TBC Warriors na Bunge SC itachezwa Juni 5 mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma kuanzia saa 10 kamili jioni