Rais : Viongozi Wanawake msitofautiane

0
209

Wakuu wa mikoa na Makatibu Tawala Wanawake wametakiwa kushirikiana wanapokuwa katika vituo vyao vya kazi na si kutofautiana.

Wito huo umetolewa Ikulu Chamwino mkoani Dodoma na Rais Samia Suluhu Hassan, wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Tawala wa Mikoa aliowateua hivi karibuni.

Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa, hategemei kuwa mkoa ambao kuna Viongozi ambao ni Mkuu wa Mkoa na Katibu Tawala wote ni Wanawake kutofautiana kwa sababu yoyote ile.

Badala yake amewataka kushirikiana na kuonesha kuwa wanaweza, ili kufuta dhana iliyojengeka miongoni mwa watu kuwa Wanawake hawaweze kufanya kazi pamoja.

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Wanawake wote ambao amekuwa aliwateua kutambua kuwa anawaamini kuwa wataenda kuchapa kazi na kuleta matokeo chanya kwa Taifa.

Amesisitiza kuwa wasiende katika maeneo yao na kazi kujibweteka na kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, kwani wakifanya hivyo watamuaibisha yeye ambaye ni Rais aliyewateua