Rais wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Camilius Wambura kuwa Kamishna wa Polisi (CP).
Pamoja na kumpandisha cheo, Rais amemteua CP Camilius Wambura kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).
Kabla ya uteuzi huo, CP Wambura alikuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.
Wakati huo huo, Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Hamad Khamis Hamad kuwa Kamishna wa Polisi (CP).
Pamoja na kumpandisha cheo, amemteua CP Hamad kuwa Mkuu wa Kamisheni ya Fedha na Lojistiki wa Jeshi la Polisi Tanzania.
Kabla ya uteuzi huo, CP Hamad alikuwa Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Makao Makuu ya Polisi Zanzibar.