Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa baadhi ya Makatibu Tawala wa Mikoa, kuwahamisha baadhi na wengine kuwabakisha katika vituo vyao vya kazi.
Pia amefanya uteuzi wa viongozi wakuu wa taasisi kama ifuatavyo;
Makatibu Tawala wa Mikoa walioteuliwa.
- Amemteua Rodrick Mpogolo kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi. Kabla ya uteuzi huo, Mpogolo alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara.
- Amemteua Dkt. Athuman Juma Kihamia kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha. Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Kihamia alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro.
- Amemteua Hassan Abbas Rugwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam. Kabla ya Uteuzi huo,Rugwa alikuwa Mkurugenzi wa Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi.
- Amemteua Dkt. Fatuma Ramadhan Mganga kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Mganga alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Mkoani Dodoma.
- Amemteua Mussa Ramadhan Chogello kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita. Kabla ya uteuzi huo Chogello alikuwa Afisa katika Ofisi ya Rais.
- Amemteua Ngusa Dismas Samike kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza. Kabla ya uteuzi huo Samike alikuwa Katibu wa Rais, Ikulu.
- Amemteua Mhandisi Mwanaisha Tumbo kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Pwani. Kabla ya uteuzi huo Mhandisi Tumbo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga.
- Amemteua Doroth Aidan Mwaluko kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida. Kabla ya Uteuzi huo Mwaluko alikuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu).
- Amemteua Balozi Batilda Salha Buriani kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga. Kabla ya uteuzi huo Balozi Buriani aliwahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya na Japan.
- Amemteua Azza Hilal Hamad kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu. Kabla ya uteuzi huo Azza aliwahi kuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga.
- Amemteua Pili Hassan Mnyema kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga. Kabla ya uteuzi huo, Mnyema alikuwa Afisa katika Ofisi ya Rais.
Makatibu Tawala wa Mikoa waliohamishwa vituo vya kazi;
- Amemhamisha Dkt. Seif Abdallah Shekillage aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro.
- Amemhamisha Karoline Albert Mthapula aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara.
- Amemhamisha Albert Gabriel Msovela aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara.
- Amemhamisha Dkt. Angelina Mageni Lutambi aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya.
- Amemhamisha Mariam Amri Mtunguja aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro.
- Amemhamisha Abdallah Mohamed Malela aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara.
- Amemhamisha Judica Haikase Omari aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa Njombe.
- Amemhamisha Denis Isdory Bandisa aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa.
- Amemhamisha Missaile Albano Musa aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe.
Makatibu Tawala wa Mikoa wanaobaki katika vituo vyao vya kazi;
- Happiness William Seneda anabaki kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa.
- Prof. Faustine Kamuzora anabaki kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera.
- Rashid Kassim Mchatta anabaki kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma.
- Rehema Seif Madenge anabaki kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi.
- Steven Mashauri Ndaki anabaki kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma.
- Msalika Robert Makungu anabaki kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora.
Watendaji Wakuu wa Taasisi;
- Amemteua William Erio kuwa Afisa Mtendaji Mkuu, Tume ya Ushindani wa Biashara (FCC). Kabla ya uteuzi huo Erio alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).
- Amemteua Dkt. John Kedi Mduma kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF). Kabla ya uteuzi huo Dkt. Mduma alikuwa Afisa Mtendaji Mkuu, Tume ya Ushindani wa Biashara (FCC).
Uteuzi huu wa Makatibu Tawala umeanza leo tarehe 29 Mei, 2021 na wataapishwa tarehe 02 Juni, 2021 saa 4:00 asubuhi, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.